AudioPlayer


-->



miujiza na baraka huja kutegemea utayari wa mtu binafsi

UTANGULIZI
waebrania 10:38
 38 Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.
 39 Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.

     VITU VINAVYO RUHUSU AU SABABISHA MTU APOKEE BARAKA NA MIUJIZA YAKE  NI :-

  • utii kwa maagizo uliyopewa na MUNGU
biblia inatuonyesha dhahili yakuwa tubalikiwa tukiwa watii katika kila jema na tuta laaniwa tukifanya kila lilo  baya kama ilivyo ainishwa katika kumbukumbu 30:14-20

14 Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako, upate kulifanya.
 15 Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya;
 16 kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda Bwana, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki.
 17 Lakini moyo wako ukikengeuka, usipotaka kusikiza, lakini ukavutwa kando kwenda kuabudu miungu mingine, na kuitumikia;
 18 nawahubiri hivi leo hakika mtaangamia; hamtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi, uivukiayo Yordani, uingie kuimiliki.
 19 Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;
 20 kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.
 pia soma kumbukumbu 28 
  • imani : kwa imani watu hupokea miujiza na baraka zao 
tukiangalia kwa baba yetu wa imani ambaye ni ibrahimu tunajifuza kuwa imani hufanya jambo lisilo wezekana liwezekane 
Mathayo 9:29 Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate.
Mathayo 17:20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
unaweza soma zaidi habakuki 2:4,luka7: 50 na marko 5:34

Hakuna maoni: