utangulizi
UTII
utii ni kukubali na kutenda jambo uliloagizwa kwa ufasaha na kwa wakati ulioamuriwa kutenda kwa kusudi maalumu pia Mungu anatuatha tuwe watii katika kutenda kazi zake kama jinsi alivyo tuagiza tukiangalia katika kitabu cha kutoka 23:22-2522 Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.
23 Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali.
24 Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande.
25 Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.
Basi jinsi vitabu vinavyo eleza kuhusiana utii kuna mambo ambayo hupata mtu akiwa mtii katika neno na kulitenda pia kuenenda katika hilo maana atakayevumilia mpaka ndiye atahesabiwa haki
kolosai 1:10,11(swahili union version bible)
10 mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;
11 mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;
REHEMA
Rehema ni hali kujinyekeza mbele za au kuomba msamaha baada ya kutambua kosa ulilotenda nakukili kuto rudia makosa zaburi 51:1-8
1 Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.
2 Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.
3 Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima.
4 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.
5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
6 Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri,
7 Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji
8 Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi.
Isaya 1:16-20
16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;
17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.
18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
20 bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya
faida za kuomba rehema
- kupata wokovu
zaburi 103:1-3
1 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu.
2 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.
3 Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,
No comments:
Post a Comment