AudioPlayer


-->



utimilifu wa sheria katika kristo upo katika upendo 
warumi 13:10

 10 Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.

 biblia inatuasa kupendana katika kristo YESU pia inaasa kuwapenda watu wote ikewemo adui zetu huku tukiwabariki  kama inavyosema 
injili ya luka 6:27-28
27 Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi,
 28 wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.
 
pia walaka wa mtume Paulo  kwa kanisa liloko korintho unazungumzia haswa sifa za upendo kama ifuatavo
  1. kutobagua
  2. kuvumilia
  3. kutohusudu
  4. kutii
  5. hujivuni
1 kor 13:1-13
 1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
 2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.
 3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
 4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
 5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
 6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
 7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
 8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
 9 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;
 10 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.
 11 Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.
 12 Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.
 13 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.

Hakuna maoni: