AudioPlayer

-->

utoaji

MAKUNDI 7 YA WATOAJI ZAKA NA SADAKA KANISANI.

1. Wanaojaribu kumpa MUNGU rushwa.

1 Samweli 15:22.
Hawa huwa hawatoi matoleo vyema hadi pale watakapobanwa na matatizo makubwa. Mfano watakapoteseka na magonjwa, watakapofilisika, watakapokuwa na kesi mahakamani au watakapokuwa na migogoro mikubwa kwenye familia zao au ndoa zao ndipo wataanza kutoa zaka sahihi na sadaka nzuri ili MUNGU awatoe katika magumu yao.
Kwanini nimesema kwamba ni kama wanataka kumpa MUNGU rushwa kitu ambacho hakiwezekani?
Ni kwa sababu wakishatolewa kwenye matatizo  hutawaona tena wakitoa vizuri hadi watakapobanwa tena.
Utoaji matoleo wa mtu wa aina hii hauwezi  kumletea baraka stahiki za utoaji wake katika maisha yake.

Dawa ni kutubu na kuanza kutoa kama MUNGU atakavyo.
Mithali 15:8

2. Kundi la pili la watoaji wa sadaka na zaka ni wale wanaotoa kwa kufuata mkumbo tu.

Kutoka 25:1-3
Maandiko yanaonyesha kwamba mtoaji sahihi atoe kwa moyo  wa upemdo na sio mkumbo.
Watu wa kundi hili hawatoi zaka sahihi au sadaka nzuri hadi watakapoona wengine wanatoa vizuri.
Kwenye michango ya kuahidi mtu wa kundi hili hawezi kuahidi  hadi atakapoona watu kadhaa wameahidi ndipo na yeye ataahidi. Ahadi yake haitoki moyoni Bali ni kufuata mkumbo.
Mtu wa kundi hili wakati wa kutoa sadaka yeye hawezi kwenda kutoa hadi atakpoona wengine wameenda kutoa.
Wakati mwingine aliokaa nao karibu Ibadani Kama hawajapeleka sadaka na yeye huacha kupeleka hata kama anayo mfukoni sadaka hiyo.
Wao hawawezi kutoa hadi waone wengine wanatoa, hata kama ROHO MTAKATIFU atawasukuma kutoa wao hawatatoa.
Mtoaji wa namna hii hawezi kubarikiwa vizuri na MUNGU hadi atakapotibia jambo hilo ndio aache kutoka vile atakavyo MUNGU.

Makundi mengine  6 yanafuata baadae ili na wewe ujione uko kundi gani.
MUNGU akubariki.MAKUNDI 7 YA WATOAJI ZAKA NA SADAKA KANISANI.

MUNGU akubariki.

Hakuna maoni: