JINSI KUFUNGA KUNAVYOBADILISHA
MAMBO
Sehemu nyingi sana katika Biblia, tunaona
jinsi ambavyo mambo yalivyobadilika
baada ya kufunga na kuomba. Angalia
mifano mitano ifuatayo:-
1. Wana wa Israeli walipigwa mfululizo
katika vita na wana wa Benyamini. Baada
ya kushindwa mfululizo, wakaamua
kufunga na kuomba (WAAMUZI 20:20-22,
24-26). Baada ya kufunga na kuomba
matokeo yakabadilika, Benyamini
wakapigwa sana, na wana wa Israeli
wakashinda vita (WAAMUZI 20:34-35, 41-45,
48). Tunaweza kuitia moto miji yote ya
Shetani tukiwa wafungaji, na siyo kinyume
cha hapo;
2. Ezra hakumtegemea mfalme, bali
alifunga, na matokeo ya kufunga yakawa
kwamba mkono wa Mungu ulikuwa pamoja
naye na yeye na wenzake wakaokolewa na
mkono wa adui (EZRA 8:21-28, 31-33). Ikiwa
Kanisa linahitaji kuokolewa kutoka katika
mkono wa adui, ni lazima liwe na
wafungaji.
3. Yehoshafati alipata taarifa za majeshi
kombaini ya Maadui waliotaka kumpiga.
Akatangaza kufunga na kuomba (2 MAMBO
YA NYAKATI 20:1-4), matokeo yake
wakashinda vita kirahisi mno kwa sifa tu (2
MAMBO YA NYAKATI 20:22-25).
4. Nehemia alivyopata taarifa za
kubomolewa kwa ukuta wa Yerusalemu na
malango yaliyoteketezwa kwa moto,
alifunga na kuomba (NEHEMIA 1:3-4), na
matokeo yake ukuta ulijengwa tena
(NEHEMIA 6:15-16).
5. Hasira ya Bwana kwa Kanisa, Taifa,
kutokana na uovu wa watu, inaweza
kufanywa kuwa AMANI kwa KUFUNGA NA
KUOMBA (1 WAFALME 21:27-29; YONA
3:7-10; EZRA 10:6).
No comments:
Post a Comment